Rais Dkt. Mwinyi ateta na Mabalozi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewasisitiza mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kuzingatia diplomasia ya uchumi na kuzitangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na mabalozi wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni kwa ajili ya nchi za Rwanda, Zimbabwe, Sweden na Msumbiji, waliomtembelea Ikulu kumuaga kabla ya kuelekea katika vituo vyao vya kazi.
Amewahimiza mabalozi hao kufanya juhudi maalumu za kuitangaza sera ya uchumi wa buluu na sekta ya utalii katika mataifa wanakokwenda ili kuvutia wawekezaji zaidi kuwekeza nchini.
Amesema Zanzibar bado inahitaji wawekezaji wengi, hususan katika sekta hizo kuu za kipaumbele, kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi kama vile uvuvi, utalii, pamoja na mafuta na gesi.
Halikadhalika, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa suala la mahusiano ya kimataifa hivi sasa limeelekezwa zaidi katika nyanja za kiuchumi, hivyo ni muhimu kwa mabalozi hao kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na nchi wanazowakilisha.
Ametaja maeneo yenye fursa za kutosha kuwa ni uwekezaji katika sekta ya bandari, ikiwemo bandari za makontena, usafirishaji wa mizigo, pamoja na mafuta na gesi.
Akizungumzia sekta ya biashara, amewaagiza mabalozi hao kuzitafutia masoko bidhaa za Tanzania, ikiwemo bidhaa za viungo zinazozalishwa kwa wingi Zanzibar, pamoja na kutangaza huduma na vivutio vya utalii ili kuwavutia watalii kutembelea Zanzibar.
Nao mabalozi hao wameahidi kuyazingatia maelekezo ya Rais Dkt. Mwinyi kama dira ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, huku wakiahidi kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza nchini.
Mabalozi walioaga ni Dkt. Habibu Kambanga (Rwanda), CP Suzane Kaganda (Zimbabwe), Mobhare Matinyi (Sweden), na CP Hamad Hamad (Msumbiji).
Rais wa Romania, Mhe. Klaus Iohannis akizungumza kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa heshima yake Ikulu Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), naye akisalimiana na Waziri Nak-Yon mara baada ya kupokelewa na Mhe. Majaliwa, wa kwanza kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwele naye akisubiria kusalimiana na Waziri Mkuu wa Korea.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. David Cleopa Msuya (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samuel Malecela (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. faraji Kassidi Mnyepe wakifuatilia Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea jijini Dar Es Salaam,Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC)
Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb.) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam